TANZANIA INA UTAJIRI WA GESI ASILIA'- MHANDISI ANTELIMI RAPHAEL



TANZANIA INA UTAJIRI WA GESI ASILIA'- MHANDISI ANTELIMI RAPHAEL

Kamishna Msaidizi wa  wa Juu wa Petroli, Wizara ya Nishati, Mhandisi  Antelimi Raphael amesema kuwa Tanzania ina utajiri wa Gesi Asilia ambapo mpaka sasa kiasi kilichogunduliwa ni futi za ujazo trilioni 55.

Amesema hayo tarehe 26 Februari 2025 jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha Joto la Asubuhi kinachoendeshwa na Kituo cha Redio cha EFM ikiwa ni muendelezo wa programu za kutoa elimu kwa umma kuhusu Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Machi 5-7 mwaka huu


Amesema nishati ya Mafuta bado inaendelea kutafutwa ingawa dalili zinaonesha kuwa kuna mashapo ya mafuta hasa kwenye Bonde la Ufa ikiwemo eneo la Eyasi Wembere

Kuhusu suala la Nishati Safi ya Kupikia amesema kuwa Wizara inaendelea kutoa elimu kuhusu matumizi ya nishati hiyo pamoja na kuangalia masuala mengine yatakayowezesha mitungi hiyo kupatikana kwa urahisi kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments