EXAUD - APONGEZA CBE KUGUSA WADAU SEKTA BINAFSI ELIMU UJASILIAMALI.

 

EXAUD - APONGEZA CBE KUGUSA WADAU SEKTA BINAFSI ELIMU UJASILIAMALI.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ,Exaud Kigahe amesema kitendo cha Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutoa elimu kwenye sekta binafsi kutawajengea uwezo wa kutambulika.

Kigahe amesema hayo leo Jumamosi Novemba 30,2024 wakati akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini ,Dk Tulia Ackson kwenye mahafari ya 59 ya Chuo cha CBE .

Amesema mafunzo ya biashara kwa sekta zisizo rasmi wakiwepo wahudumu wa mabasi,bodaboda ni kuibua ufanisi na kutambulika kwa mujibu wa sheria .

"Pia nimeona CBE mmeboresha mitaala na miundombinu chuoni hapa ikiwepo bwalo la chakula ambalo leo nimelikagua na Spika wa Bunge Dkt Tulia atafika kutembelea na kulizindua"amesema.

Aidha amepongeza uongozi wa chuo kwa kuongeza mashirikiano na mataifa mengine sambamba na kuanzisha programu ya uanagenzi ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

"Mitaala hiyo itawezesha vijana kupata nafasi za kuanza kujitegemea hivyo nisisitize Taasisi zote za elimu ya biashara kuwekeza katika bunifu hatamizi na uanagenzi ili kufikia uchumi wa kati na juu zaidi "amesema.

Amesema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira wezeshi na mashirikiano na Taasisi nyingine kuona vijana wanapata elimu bora na kujiajiri .


Mkuu wa Chuo ,Profesa Edda Lwago amesema katika kuboresha tafiti Chuo kimeshirikiana na mashirika kutoka mataifa mbalimbali ili kusaidia kuboresha tafiti.

Amesema CBE wameanza kuwajengea uwezo vijana wa elimu ya sekondari kujifunza stadi za biashara kwa kaunzisha klabu mashuleni.


Makamu Mwenyekiti wa bodi ya chuoni hapo hicho,Dkt,Kenedy Hosea amesema CBE imetoa kipaumbele kuwajengea uwezo vijana kupata elimu ujasiriamali ili kujiajiri sambamba na kuomba wizara kukiwezesha kuanzisha programu nyingine.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments