MASACHE AWAPA KICHEKO WALIMU CHUNYA ATOA MITUNGI YA GESI 115 MASHULENI



MASACHE AWAPA KICHEKO WALIMU CHUNYA ATOA MITUNGI YA GESI 115 MASHULENI

Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amekabidhi mitungi ya nishati safi ya gesi 115 kwa walimu kwa ajili ya matumizi kwa shule za msingi na sekondari jimboni kwake.

Masache amekabidhi mitungi hiyo leo Novemba 30,2024 Mara baada ya kuwa mgeni rasmi kwenye Bonanza la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ngazi ya Mkoa lililofanyika katika viwanja vya Sinjilili wilayani humo.

Amesema amewiwa kutoa mitungi ya nishati safi mashuleni lengo ni kuwa mabalozi wa kuhamasha jamii kuachana na matumizi ya nishati chafu ya mkaa.

" Kwa kutambua Wilaya ya Chunya ni miongoni mwa maeneo yaliyo athirika sana na uharibifu wa mazingira hivyo utoaji wa nishati hiyo ni kuwezesha kupeleka ujumbe wa kutunza mazingira na kuunga mkono kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhasisha matumizi nishati safi "amesema


Masache amesema kwa awali hii ya kwanza zimenufaika Shule za msingi 90 na Sekondari 19 kwa ajili ya matumizi mbalimbali muhimu na kwamba mitungi hiyo ina thamani ya Sh 5.1 milioni

Pia Mbunge huyo ametoa jezi seti 10 kwa ajili ya kuhamasisha michezo katika Wilaya sita za Mkoa wa Mbeya

Mwisho

Post a Comment

0 Comments