MIAKA 20 JELA KWA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI



MIAKA 20 JELA KWA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI

Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Lindi imemukumu Said Selemani Litangulu (55) huku ikiwaachia huru watuhumiwa wawili Bakari Said Litungulu (32) na Selemani Hassani Litangulu (22) wote wakazi wa kijiji cha Nakiu wilaya ya Kilwa ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa matatu ya kupatikana na Nyara za Serilali (Meno ya tembo mazima 28 na vipande 62, kosa la pili Kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali huku kosa la tatu likiwa ni Kujihusha na  kusafirisha nyara za SerikalI.

Mtuhumiwa namba moja ambaye ni Saidi Selemani Litungulu alishtakiwa kwa makosa mawili, kosa la kwanza Kupatikana na nyara za Serikali, kosa la pili kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali na mtuhumiwa namba mbili Bakari Saidi Litungulu na namba tatu Selemani Hassani Litunguli wakishtakiwa kwa kosa moja la kusafirisha nyara za Serikali.

Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti mtumiwa namba moja alikamatwa Machi 30, 2023  mtuhumiwa namba mbili na tatu walikamatwa Aprili 04, 2023 wote katika kijiji hicho cha Nakiu na kufikishwa katika mahakama hiyo Aprili 17, 2023.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba ECO 4 ya mwaka 2023 hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Consolata Singano alisema mahakama imemkuta mtuhumiwa namba moja na hatia kwa kosa moja la Kupatikana na Nyara za Serikali.

Ambapo Mahakama hiyo imemfutia kosa namba mbili la kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali kwa kile alichosema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha ukweli  mtuhumiwa huyo kujihusisha na biashara hiyo na ikampatia adhabu kwa kosa la kwanza kwenda gerezani kutumikia adhabu ya miaka 20 au kulipa faini ya shilingi  10,754, 000,000 na kutaifisha kielelezo hicho cha meno 28 na vipande 62 vya meno ya Tembo, mali yake ya pikipiki aina ya boxa pamoja na simu tatu za mkononi aina ya Teckno.

Mtuhumiwa namba mbili na tatu mahakama iliwaachia huru kwa kuwa mashahidi upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha ukweli wa makosa walishtakiwa nao.

Upande wa mashtaka ulikuwa hukiongozwa na Godfrey Mramba na Denis Nguvu ambapo ulipeleka jumla ya mashidi 10 na vielelezo 21 huku upande wa utetezi ukipeleka mashahidi 7

Post a Comment

0 Comments