MASACHE: AMLILIA MWENYEKITI UVCCM ALIYEUWAWA CHUNYA

 

MASACHE: AMLILIA MWENYEKITI UVCCM ALIYEUWAWA CHUNYA

Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amelitaka Jeshi la Polisi kujitafakari kufuatia kujirudia kwa matukio ya  mauaji ya likiwepo la Mwenyekiti wa UVCCM Mtaa wa Machinjioni Kata ya Makongorosi Michael Kalinga .

Masache ametoa kauli hiyo leo Desemba 3,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi  baada ya kupokea  taarifa za mauaji ya  Michael  Kalinda.

Amesema katika Wilaya ya Chunya Mji wa Makongorosi umekuwa na matukio ya mauaji ya kujirudia na kusababisha jamii kuishi kwa hofu na kuomna suala lishughulikiwe haraka.

Wakati huo huo Masache amesema amepokea taarifa za mauaji hayo kwa masikitiko na kueleza alishiriki kikamilifu na kufanikisha zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27,2024.

Kaimu Kamanda wa Polisi  Kamishna wa Polisi ,Wilbert Siwa amethibitisha kutokea  tukio hilo na kwamba  wanaendelea na kulifuatilia .

Amesema  taarifa za awali zimeeleza Marehemu alikuwa raia wa kawaida na sio kiongozi wa Chama.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments