MASACHE AUNGANA NA WAOMBOLEZAJI MAZISHI MWENYEKITI UVCCM CHUNYA


 MASACHE AUNGANA NA WAOMBOLEZAJI MAZISHI MWENYEKITI UVCCM CHUNYA.

Mbunge wa Lupa Masache Kasaka ameungana na waomboleza katika mazishi ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Tawi la Machinjioni Kata ya Bwawani,Michael Kalinga (36) huku akikemea matukio .

Kalinga aliuwawa usiku wa kuamkia Desemba 3,2024 kwa kupigwa na kitu butu kichawani katika eneo la Mihanzini Kata ya Mkola Wilaya ya Chunya.

Akizungumza na maelfu ya wananchi walioshiriki mazishi hayo , Mbunge Masache amemtaja marehemu alikuwa na mchango mkubwa kwa chama na serikali.

"Nitoe pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu huu ni msiba huo ,lakini waliohusika na mauaji waliona wamejificha lakini mbele za Mungu walionekana na ndio maana wamekamatwa "amesema Masache.

Masache amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ya kuwabaini waliohusika na kuomba kuendelea kulinda hali ya amani na utulivu ili kuendelea kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zilizopo.

Mwandishi wetu- Mbeya

Post a Comment

0 Comments