MPANGO WA KUWALINDA WATU WENYE UALBINO KUZINDULIWA DISEMBA 3, 2024


 MPANGO WA KUWALINDA WATU WENYE UALBINO KUZINDULIWA DISEMBA 3, 2024.

#KAZIINAONGEA

Kwa kipindi kirefu jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) imekuwa ikiishi kwa kukosa amani kwa hofu ya kuuawa na viungo vyao kutumiwa kwa imani potofu za kishirikina, Serikali ya Awamu ya Sita imekuja na mpango kazi wa Taifa wa haki na Ustawi kwa watu wenye Ualbino.

Mpango huu wa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, utasaidia kuwawekea mazingira mazuri watu wenye Ualbino pamoja na kukuza uelewa katika jamii juu ya watu wenye Ualbino.

Mkakati huu wa Kitaifa wa Teknolojia Saidizi kwa watu Wenye Ulemavu ulioandaliwa na Serikali, unatarajiwa kuzinduliwa Disemba 3, 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema, Serikali imekamilisha uandaaji wa Mpango kazi huo wa Taifa na baada ya kuzinduliwa utekelezaji utaanza.

Aidha, Ridhiwani amesema hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa matembezi ya hisani ya kukuza uelewa kuhusu Watu wenye Ualbino na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kundi hilo.

Harambee hiyo ya ukusanyaji fedha, itasaidia kundi la watu hao na kwamba mpango huo utaandaa miongozo itakayosaidia kuwalinda Watu Wenye Ualbino.

Hatua ya kuwalinda watu wenye Ualbino ni jambo linalopaswa kutelelezwa na makundi yote ya jamii na kwa upande wa Serikali, imeweka hatua kadhaa ambazo utekelezaji wake utahusisha ngazi mbalimbali za Serikali, Viongozi wa dini pamoja na watoa tiba za jadi.

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments