Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must) kimesema kimeanza mchakato wa kutenga maeneo kwa ajili ya kufanya tafiti za kisayansi katika sekta ya kilimo .
Makamu Mkuu wa Chuo Must , Profesa ,Aloys Mvuma jana Desemba 4,2024 kwenye mdahalo wa wazi wa kujadiliana changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na kuja na suluhisho la kudumu sambamba na kufungua ndaki ya mafunzo ya kilimo cha kisayansi shirikishi na bunifu.
Profesa Mvuma amesema mdahalo huo umehusisha wanafunzi wahadhiri na mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia,kilimo na lishe, kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Profesa, Benard Chove ikiwa ni kuelekea mahafari Desemba 6,2024.
Amesema lengo ni kuhamasisha Wahadhiri na vijana kutenga maeneo ya tafiti za kisayansi kwa ajili ya kupata mwarobaini wa kukabiliana na athari hiyo ambayo imekuwa changamoto katika sekta ya kilimo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo ,taaluma,utafiti ushauri wa kitaaluma Profesa , Godliving Mtui amesema wamejidhatiti kuhakikisha tafiti zinazo zalishwa kuleta suruhisho katika jamii .Amesema kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na kwamba kabla ya kufanya tafiti wamekuwa na mfumo wa kuandika mawazo ya maeneo husika ya kimkakati.
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Sokoine (SUA) , na mbobezi wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi,kilimo na lishe,Profesa Benard Chove,ametaka maofisa ugani wa serikali kutumia tafiti zilifanywa ili kupata suruhisho la kudumu.
"Mabadiliko ya tabia nchi yameleta madhara makubwa ya kuzalisha hewa chafu ya okaa ambayo uenda kuathiri mazao yaliyopandwa na kusababisha kutokuwa na ubora unaoweza kuboresha lishe ,"amesema.
0 Comments