NMB WATOA VIFAA VYA SHULE VYENYE THAMANI YA SH.MILION 23.7 JIMBO LA MUFINDI KUSINI
Na Mwandishi wetu, Iringa
Upungufu wa madawati katika shule za msingi za Kasanga, Kisasa na Sawala Jimbo la Mufindi kusini umeanza kutatuliwa baada ya Bank ya NMB kutoa msaada wa madawati 150 na bati 150 vyenye thamni y sh 23.7 Milioni.
Akizungumza wakati akitoa vifaa hivyo chief Internal Audit kutoka Makaa Mkuu ya NMB Benedicto Baragomwa amesema kuwa kutokana na changamoto ya madawati katika shule hizo wametoa idada ya hiyo madawati kwa shule hizo tatu huku bati 150 zikiwa za shule ya msingi Kasanga kwa ajili ya ujezi ambao bado unaendelea.
Chief huyo ametaja idadi ya madawati ambayo wamekabidhi katika shule hizo kuwa shule ya Msingi kasanga madawati 50 na shule ya Msingi Kisasa dawati 50 huku shule ya Msingi sawala wakikabidhiwa dawati 50
Baragomwa amesema kuwa NMB wamekuwa wakifanya hivyo kila wakati kwa malengo yao kurejesha sehemu ya faida ambayo wanaipata kwa jamii kutokana na kazi nzuri ambayo tawi la mafinga wanaifanya.
“Bank ya NMB inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali awamu ya sita inaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia kwa kutoa fedha nyingi ili wapate mazingira bora ya kufundishia kwa wanafunzi ili wapate elimu bora ndio msingi wa maendeleo kwa taifa lolote.” Amesema Baragomwa
Aidha Baragomwa Ameshukuru viongozi wa wilaya pamoja na halmashauri kwa ushirikiano ambao wamakuwa wakiupata huku akisema kuwa kati ya matawi ya Bank ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini ambayo yanafanya vizuri tawi la Mafinga ni mojwapo.
“Hali hii inathibitisha na kuonyesha kwamba kuna kazi kubwa ambayo inafanyika pamoja na mzunguko wa fedha mkubwa katika eneo hili na ushirikiano wa viongozi wa wilaya pamoja na halmashauri uliopo ili kubadirisha hali na mazingira bora ya kujifunza na kujisomea kwa wanafunzi hao.” Amesema Chief huyo
Pia Kiongozi huyo Mbali ya kukabidhi madawa hayo lakini Chiefu huyo ameihidi kutoa madawati mengine 110 kwa shule ya masingi kasanga ili kumaliza kabisa changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini na Naibu waziri wa uchukuzi David KIenzila ameshukuu kwa msaada huo uliotolewa na bank hiyo huku akuimba NBM kusaidia katika shule ya msingi kisasa kukarabati wa shule hiyo kutokana na miundombinu yake kuwa chakavu.
“Tuna shukuru kwa msaada huu wa madawati kwa shule hizi pamojna na mabati baada ya kutoka hapa kwa ajili yaa kwenda kuangalia shule ya kisasa kufanyiwa ukarabati wa shule hiyo kwa sababu kuna hali mbaya ya madarasa katikaa shule hiyo.” Amesema Kienzile
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Afisa Tawala wa wilayani Robart Kiwero amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya Elimu ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kujifunzia.
"hata nyinyi ni mashaidi shule za vijijini na Mijini zote zipo sawa Nchini Nzima kwa sbabu ameona thamani kwa watu ambao wapo mikoani ikwemo vijijini na mijini ni sawa kwani wote tunahitaji elimu iliyobora .” Amesema Kiwero
Mwisho
0 Comments