RAIS SAMIA AAHIDI 'KUIPIGANIA' NAFASI YA DKT. NDUGULILE WHO


RAIS SAMIA AAHIDI 'KUIPIGANIA' NAFASI YA DKT. NDUGULILE WHO

#KAZIINAONGEA 

Katika kuhakikisha heshima ya Tanzania inasalia katika kiwango chake kimataifa, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa serikali yake itaweka nguvu ile ile katika kupigania nafasi ya Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika aliyoiacha marehemu Dkt. Faustine Ndugulile.

Rais ameyasema hayo Desemba 2, 2024 wakati akitoa salamu za pole kwenye shughuli maalumu ya kuuaga mwili wa mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

“Katika safari yake hii ya mwisho Dkt. Ndugulile ameweka heshima kubwa kwa nchi yetu kwa kupata nafasi ile, na niseme kwamba Mungu amechukua amana yake, lakini kwetu sisi ni kwenda mbele, tutaingia tena kwenye ushindani wa nafasi ile, tutatafuta Mtanzania mwenye sifa zinazoweza kushindana na ulimwengu, tutaingia tena na tutaweka nguvu ileile ili kuweka heshima ya nchi yetu.”

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments