RAIS SAMIA APONGEZWA KUKUTANA NA WAKAZI WA NGORONGORO


RAIS SAMIA APONGEZWA KUKUTANA NA WAKAZI WA NGORONGORO

#KAZIINAONGEA

Ni kiongozi msikivu, mwenye huruma, asiyependa uonevu na mwenye kutaka haki. Ni Rais Samia Suluhu Hassan ambae tangu aingie madarakani amekuwa akiishi falsafa yake ya 4R.

Falsafa hii inalenga Maridhiano, Ustahimilivu, Maboresho na kujenga upya, kupitia falsafa yake hiyo Desemba 1,2024 Rais Samia alikutana na wakazi wa Ngorongoro.

Hatua hiyo imeonekana kuwavutia wengi na kuamua kumpongeza kwa kuiona haja ya kulimaliza sakata la Ngorongoro kwa njia ya maridhiano.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa amekuwa miongoni mwa watu waliompongeza Rais Samia.

Aidha, Olengurumwa amempongeza Rais kwa hatua ya kukutana na watu wa Ngorongoro, na kusema kuwa, imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa watu hao, na anashukuru angalau sasa amekutana nao.

Rais Samia amesema ataunda tume mbili kuchunguza kinachojiri Ngorongoro na kusababisha kuwapo kwa malalamiko kwa wakazi wa eneo hilo.

Amesema tume moja itachunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangalia utekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Samia ameyasema hayo katika Ikulu Ndogo ya Arusha wakati akizungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai (Malaigwanani) wanaoishi Ngorogoro. 

Taarifa iliyotolewa kwa umma na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais-Ikulu ilieleza kuwa mkutano huo ulifanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kufuatia kuwapo malalamiko dhidi ya baadhi ya uamuzi wa serikali unaohusu eneo la Ngorongoro.

Hata hivyo Rais Samia amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya serikali na jamii hiyo.

Vilevile, amesisitiza ulazima wa wananchi kushirikishwa ipasavyo katika upangaji na utekelezaji miradi inayopita kwenye maeneo yao.

Ameongeza kuwa, Tanzania ni nchi inayojivunia umoja wa kitaifa na yenye serikali inayowahudumia Watanzania wote. Hivyo, akaitaka Ofisi ya Rais - TAMISEMI kushughulikia changamoto zinazojitokeza ikiwamo kukosekana kwa baadhi ya huduma za msingi za kijamii katika eneo la Ngorongoro.

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments