SAMIA INFRASTRUCTURE BOND NI RAFIKI KWA WATANZANIA WOTE

 

SAMIA INFRASTRUCTURE BOND NI RAFIKI KWA WATANZANIA WOTE

#KAZIINAONGEA

1.Mtu yeyote au kundi au taasisi anaweza kununua  Samia Infrustructure Bond.

2.Kununua kiwango cha chini ni kuanzia 500,000 na kuendeleaa.

3.Bond inanunuliwa kupitia benki ya CRDB na kupitia simu yaani simbanking App kwa urahisi kabisa.

4.Kipindi cha mnada wa bond hii kitakuwa ni mwezi mmoja.

5.Riba kwa mwaka itakuwa ni asilimia 12.

6.Bond hii itaiva (mature) baada ya miaka mitano na baada ya muda huo wa  miaka mitano mtaji wa mteja utarudishwa.

7.Riba itagawiwa kila robo mwaka yaani baada ya miezi 3.

8.Bond hii haina kodi hivyo riba yako utapewa kama ilivyo bila makato yoyote.7

9.Bond hii haina gharama za uendeshaji zozote kwa mteja.

10.Pesa itakayokusanywa italipa mikataba ya wakandarasi na TARURA kwa mikataba ya sasa na mipya

Na malipo kwa wakandarasi yataanza Februari ,2025 baada ya mnada wa bond kukamilika.

11.Ukiwa na bond ya Mama Samia,utaitumia kama dhamana  kupata mkopo wa mpaka 80% ya mtaji wako kutoka CRDB Bank.

Kama ilivyoelezwa bond hii  mnufaika ni TARURA kwa maana ya kuwezesha malipo ya wakandarasi,  tunahimizwa kuhamasisha watu,jamaa,marafiki,vikundi sogozi kununua bond hii kwa maendeleo ya Taifa letu.

@KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments