SERIKALI YA SAMIA KUKARABATI MADARAJA MAKUBWA MANNE USHETU

 

SERIKALI YA SAMIA KUKARABATI MADARAJA MAKUBWA MANNE USHETU

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kurekebisha miundo mbinu ya madaraja iliyoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha katika nyakati tofauti nchini.

Tayari imepanga kutumia kiasi cha shilingi bilioni 18.05 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja makubwa manne ya Ubagwe, Kasenga, Ng’hwande na Mwabomba yaliyoathiriwa na mvua hizo katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.

 Ujenzi wa madaraja hayo utatekelezwa na wakandarasi wazawa kutoka Kampuni ya Salum Motors na Jonta Investment ambao wamekabidhiwa kazi hiyo tangu Novemba 30, 2024

Ujenzi wa Daraja la Ubagwe (m 40) utagharimu Bilioni 4.14, Daraja la Kasenga (m 60) utagharimu bilioni 5.13, Daraja la Ng’hwande (m 40) utagharimu billion 4.28 na Daraja la Mwabomba (m 50) utagharimu bilioni 4.5 pamoja na ujenzi wa tuta la barabara (m 300) kwa kiwango cha changarawe katika kila daraja, kwa muda wa mwaka mmoja.

Ujenzi wa madaraja hayo ukikamilika utaondoa changamoto na adha ya usafiri kwa wananchi waliyokuwa wakiipata kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara katika kila msimu wa mvua kubwa.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments