SERIKALI YA SAMIA YAPELEKA MAJIKO YA GESI ZAIDI YA 400,000 KWA WANANCHI

 

SERIKALI YA SAMIA YAPELEKA MAJIKO YA GESI ZAIDI YA 400,000 KWA WANANCHI

*●Kagera yapata majiko 22,785* 

#KAZIINAONGEA

Katika kufanikisha Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia kuwafikia watanzania wengi zaidi, Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imepanga kusambaza zaidi ya majiko 400,000 nchi nzima, yatakayouzwa kwa bei nafuu.

Tayari mkoa wa Kagera umeshapatiwa majiko 22785 ambayo yatauzwa na mawakala maalum walioteuliwa.

Hivi karibuni Wakala wa Nishati vijijini -REA- walitambulisha mradi wa kuuza majiko ya gesi ambayo yana ruzuku ya Serikali kwa mkoa huo.

Majiko hayo yana  thamani ya shilingi milioni 398 na yatauzwa kwa uwazi kwa kila mwananchi mwenye uhitaji.

Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo kwa uongozi wa mkoa wa Kagera ,Meneja mradi wa nishati safi kutoka REA,  Mhandisi Deusdedit Malulu amesema kuwa mradi huo utatekelezwa nchi nzima ambapo utawezesha wananchi kuepuka uharibifu wa misitu kwa kukata miti na kuchoma mkaa na utafutaji wa kuni.

Amesema mradi huo utasaidia kuongeza kasi ya utunzaji wa mazingira.

Mhandisi Malulu ameongeza kuwa kwa Tanzania nzima wanatarajia kutoa majiko  400,052 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.6 ambayo yatakuwa yakiuzwa kwa wananchi kwa gharama nafuu ya shilingi elfu 17,500, lengo likiwa ni kila mwananchi kutumia nishati safi wakati wa kupika chakula.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Kagera Stephen Ndaki ameishukuru REA kwa kuleta mradi huo Kagera na kusema kuwa anaomba uanze mara moja kwani  Kagera inao uhitaji mkubwa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments