TANZANIA KINARA WA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI
#KAZIINAONGEA
Uamuzi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuifungua nchi kiuchumi umesaidia kuifanya Tanzania kuwa kinara wa biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Ukweli wa hilo umethibitishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto.
Akiongea katoka mjadala wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuadhimisha miaka 25 uliofanyika jijini Arusha, Ruto amesema awali nchi yake ndio ilikuwa inaongoza kufanya biashara ndani ya jumuiya hiyo, lakini sasa hali ni tofauti.
"Kenya ndio ilikuwa ikiongoza kufanya biashara ndani ya jumuiya yetu, lakini leo Tanzania ndio imekuwa kinara, hii ni hatua kubwa kwa Tanzania na nawapongeza kwa hili.
"Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunaitumia jumuiya hii kujiimarisha kiuchumi."
Tanzania imefanikiwa kushika usukani wa biashara ndani ya EAC na kikanda kwa sababu ya kuboresha mazingira ya kibiashara na kuvutia wawekezaji zaidi.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments