UBELGIJI YAVUTIWA NA TANZANIA KIBIASHARA

 

UBELGIJI YAVUTIWA NA TANZANIA KIBIASHARA

#KAZIINAONGEA

Mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameivutia Ubelgiji kushirikiana na Tanzania kwenye biashara na uwekezaji.

Ushirika huo unakuja baada ya hivi karibuni Tanzania kuwakaribisha kwenye kongamano la wawakilishi kutoka kampuni za Ubelgiji zinazotafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini.

Kupitia kongamano hilo lililowezesha majadiliano kati ya serikali na ushirikishwaji wa biashara, lilitoa jukwaa kwa wananchi wa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na kuunda umoja katika sekta muhimu za kiuchumi kama vile kilimo na biashara.

Hafla hiyo iliwaleta pamoja wawakilishi kutoka kampuni 40 za Ubelgiji na zaidi ya kampuni 350 za ndani na kupata nafasi ya kujadili na kutafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

Aidha jukwaa hilo linaendana na juhudi kubwa za serikali ya awamu ya sita za kukuza uwekezaji, kufikia uchumi wa viwanda, kutengeneza ajira, kukuza teknolojia na kusukuma maendeleo ya uchumi wa nchi.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments