BARAZA LA MADIWANI LAIDHINISHA BAJETI YA BILION 108 MIRADI YA MAENDELEO


BARAZA LA MADIWANI LAIDHINISHA BAJETI YA BILION 108 MIRADI YA MAENDELEO

Mbeya .Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Mbeya limeidhinisha bajeti ya zaidi ya Sh 108 bilioni kutumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka 2025/26.

Sambamba na bajeti hiyo limefanikiwa kuvuka malengo ya makusanyo mapato ya ndani kutoka Sh 21.9 bilioni mpaka Sh 2.3 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2024/25 mpaka 2025/26.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwaji Mstahiki Meya Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema kutokana na mapato ya ndani kuongezeka wanataraji kutumia zaidi ya Sh 8 bilioni kuboresha miundombinu ya elimu na kukarabati shule kongwe .

Amesema kimsingi wanahitaji shule zote za jiji la Mbeya kuwa za kisasa na muonekano mzuri ili kuwa kivutio kwa wanafunzi.

Ametolea mfano kwa Shule ya msingi Ilomba iliyopo Kata ya Isyesye iliyojengwa mwaka 1953 tayari waliitengea bajeti ya Sh 150 milioni na kuifanyia ukarabati mkubwa


Ametaja baadhi ya shule nyingine kongwe zilizofanyiwa ukarabati miundombinu ni Isanga ,Muungano,Mapinduzi zikiwa ni miongoni mwa 87 katika Jiji la Mbeya zitakazo kuwa na muonekano mzuri .

Amesema licha ya kuwa ni maelekezo ya serikali ,lakini pia ni kumpa heshima Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini,Dk Tulia Ackson .

"Tunashuhudia Dk Tulia amekuwa kipaumbele kusukuma uwekezaji katika nyanja mbalimbali ikiwepo sekta ya elimu itakuwa aibu anakuja na wageni wa kitaifa hali ya shule zetu zinahatarisha usalama wa wanafunzi,"amesema

Diwani Kata ya Iyunga ,Mwajuma Tindwa amesema bajeti walipitisha mbali na sekta ya elimu imegusa nyanja mbalimbali lengo ni kuona Jiji la Mbeya linapiga hatua katika maendeleo.

Post a Comment

0 Comments