#KAZIINAONGEA
Mmoja wa wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Katibu NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Amos Makala amesema kuwa chama hicho kimejipanga na kipo tayari kushinda Uchaguzi Mkuu 2025.
Makala amesema hayo katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, ulioanza Januari 18, 2025 jijini Dodoma, unaotarajiwa kuisha Januari 19,2025.
“Chama cha Mapinduzi tumejipanga yeyote huko, pamoja na migogoro yao tupo tayari kwa yeyote na CCM ipo tayari kushinda uchaguzi wa mwaka huu”. Amesema Makala.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments