CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI TANZANIA WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA UZALISHAJI WA ZAO LA KOROSHO TANDAHIMBA
Na Mwandishi wetu, Mtwara
Wakufunzi na Wanafuchuo wa chmkoa ewa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) wakiongozwa na Mkuu wa msafara Mkufunzi Mwandamizi Elekezi Jeshi la Anga Brigadia Jenerali Erick Mhoro leo Januari 16,2025 wamefanya ziara Wilaya ya Tandahimba kujifunza uzalishaji wa zao la Korosho.
Akiwasilisha taarifa fupi ya Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele ametumia nafasi hiyo pia kuwakaribisha kuwekeza Tandahimba katika sekta ya kilimo hususani viwanda.
Katika ziara yao wakiwa Tandahimba wametembelea shamba la mkulima wa korosho kijiji cha Mivanga Kata ya Nambahu Ndg Muhdin Jumbe anaemiliki ekari kumi za shamba la mikorosho ambapo aamewaelezea jinsi alivyofanikiwa kuinua uchumi wa familia kupitia zao la Korosho.
Aidha wametembelea chama cha Msingi Matogoro ambapo wameelezwa na kuona jinsi chama hicho kinavyopokea korosho za mkulima hadi hatua ya kupeleka korosho hizo kwenye Chama Kikuu cha Ushirika na kuhitimisha ziara yao kwa kutembelea kiwanda cha Korosho cha AMAMA na kuona jinsi wanavyoiongezea thamani Korosho na kuuza Nje ya Nchi kutoka moja kwa moja Tandahimba
Kwa upande wake Brigedia Jenerali Erick Mhoro amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kwa usimamizi wa shughuli za uzalishaji wa Korosho katika Wilaya ya Tandahimba ambapo ni utekelezaji wa sera ya Serikali katika kuinua Uchumi lakini pia wamepongeza juhudi zote zinazofanyika,katika maeneo waliyotembelea .
0 Comments