DC BOMBOKO AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA STENDI YA MAGUFULI
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko na Kamati yake ya Usalama wametembelea katika Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam na Kukagua Miundombinu ya Stendi hiyo, hali ya upatikanaji wa Maji na Umeme.
Mteule huyo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea na utekelezaji wa kauli mbiu ya Kazi iendelee inayotekelezwa na watendaji na wateule wote wa Rais nchini ili kuendeleaza ujenzi wa Taifa.
Aidha Bomboko amepata wasaa wa kukagua maeneo maalumu waliyotengewa wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga wenye vitambulisho vya ujasiliamali na kuwataka wafanya kazi bila hofu.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments