DC CHUNYA AAGIZA UANZISHWAJI MFUKO WA MAJANGA WAKULIMA WA TUMBAKU .
Mwandishi wetu,Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Chunya ,Mbarak Batenga ameagiza uanzishwaji wa mfuko wa bima ya majanga kwa wakulima wa za la tumbaku.
Batenga ametoa kauli hiyo jana wilayani humo mara baada ya mvua kubwa ya mawe kunyesha na kuharibu Ekari 120 za zao la tumbaku zilizolimwa na wakulima 31.
Mkuu huyo wa Wilaya aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama mpaka vijiji ambavyo vimekumbwa na janga hilo na kutoa pole kwa wakulima.
Batenda ameagiza kuundwa mfuko maalumu wa majanga kwa wakulima ili kuwasaidia kukabiliana na hasara zinazo tokana na maafa mbalimbali.
"Mfuko huo utasaidia kupunguza hasara anayoweza kuipata mkulima kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hususani mvua nyingi" amesema.
Amefafanua kuwa yapo majanga ambayo tunaweza kuyazuia na mengine hatuwezi kuyazuia, lakini kuna namna ya kuyapunguza kwa kuweka mipango mizuri.
" Sasa maelekezo yangu kuundwe mfuko rasmi wa kushughulikia majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza ili kuwasaidia wakulima," amesema.
Ofisa Bodi ya Tumbaku Mkoa wa Kitumbaku Chunya , Loysujaki Kimiri amesema tathimini bado inaendelea mpaka sasa wakulima 31 wamepata maafa
Mwisho
0 Comments