DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU NMB
Dodoma 📍
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, akiwa na viongozi wengine wa Benki ya NMB, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko, jijini Dodoma.
Kupitia mazungumzo hayo, uwakilishi wa Benki umetoa Salamu za Mwaka Mpya 2025, kushukuru Wizara kwa ushirikiano tunaoendelea kuupata, taarifa ya maendeleo na mafanikio ya Benki ya NMB kwa mwaka 2024, kuonyesha muelekeo wa Benki yetu na Mkakati wake wa Mwaka 2025 unaolenga kutoa huduma bora kwa wateja wetu, na vilevile tumepokea mrejesho wa huduma zetu.
Benki ya NMB imepata mafanikio makubwa katika sekta ya kifedha kwa mwaka 2024, ikiwa ni pamoja na:
➡️ Kuwa Benki ya kwanza Afrika Mashariki kuorodhesha Hati fungani ya Uendelevu kwenye soko la Hisa la London na utoaji wa huduma bora za kifedha kwa wananchi.
➡️ Benki imetambuliwa na Jarida la Euromoney kama Benki bora zaidi Tanzania kwa mara ya 11 kwenye miaka 12.
Kwa 2025, Benki yetu imeahidi kushirikiana na Serikali kwa maendeleo ya sekta ya Nishati
0 Comments