#KAZIINAONGEA
Rais Samia Suluhu Hassan, ameipongeza timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kwa kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Katika kuwatia motisha wachezaji wa timu hiyo Rais Samia ameahidi kutoa fedha za goli la mama kwa kila goli litakalofungwa na Zanzibar Heroes.
Pongezi hizo amezitoa kwenye ukurasa wake wa WhatsApp channel hivi karibuni ambapo ameandika: Ninaipongeza Zanzibar Heroes kwa kufanikiwa kufika hatua ya fainali ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Mmejitoa, mmejituma na sote tunajivunia safari yenu hadi sasa.
Mchezo huu wa fainali ni nafasi ya kipekee kwenu kuandika historia, nasi tuko nyuma yenu kuwaunga mkono.
Ninawatakia kila la kheri, na ninawaahidi katika mchezo huu wa fainali Goli la Mama litakuwepo.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments