HALMASHAURI MTAMA WATENGA BILIONI 7.9 MIRADI YA KIJAMII


MADIWANI MTAMA WATENGA BILIONI 7.9 MIRADI YA KIJAMII

Mwandishi wetu, Lindi

Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi imetenga bajeti ya Sh.7 9bilioni kwaajili ya shughuli za kijamii ikiwemo,ujenzi wa shule za Sekondari,ukarabati wa vyumba vya madarasa vya shule za Msingi,stendi ya mabasi pamoja na soko la kisasa.

Akizungumza kwenye baraza la madiwani robo ya kwanza ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama Anderson Msumba amesema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Mtama imepokea kiasi cha Sh.7.9Bilioni kutoka kwenye Ruzuku ya Serikali pamoja na wahisani,ambapo fedha hizo zimepelekwa kwenye Elimu Sekondari na Elimu msingi.

Ameendelea kusema kuwa kwenye elimu Sekondari wameshatenga fedha kwaajili ya shule za kata mbili ,nyangao na Ingawali shule ya sekondari kiwalala ,na shule ya sekondari ya amali ,pia amesema kutakuwa na ukarabati wa shule za msingi ,ili kusaidia wanafunzi wanaosoma mbali wapunguze mwendo wa kwenda shuleni.

"Wanafunzi wengi wanachelewa kufika shuleni kutokana na umbali uliopo kati ya makazi yao na shule zilipo ,fedha tulizopata Sh.7.9Bilioni tayari tumeshaanza kujenga shule za sekondari za kata ili mwezi wa tatu wanafunzi waanze kusoma ,na itasaidia kuwapunguza umbali wa kwenda shule,Amesema Msumba 

Amesema pia mwanafunzi anatembea umbali wa km hadi 30 kufuata shule nilazima mwanafunzi achelewe kuripoti shule,lakini sasa hivi shule wanazokwenda kuzijenga zitapunguza umbali na wanafunzi watasoma vizuri.


Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amewataka madiwani na watendaji kushirikiana kwenda kuhamasisha wanafunzi ambao bado hawajaripoti wanaripoti wote.

"Ninachoomba viongozi wenzangu kwenda kuhamasisha wanafunzi waende shule,mim hii namba sijaipenda kabisa,hadi sasa ni wanafunzi 293 tu kati ya wanafunzi 2516 ni namba ndogo sana sijaridhishwa nayo."Amesema DC Mwanziva.

Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Mwinjuma Mumini amesema kuwa baadhi ya wanafunzi kutoripoti shuleni kumechangiwa na mambo mengi ikiwemo umbali wa wanafunzi wanapoishi na shule zilipo,ambapo pia amesema kuwa Halmashauri imejipanga kuanzia mkurugenzi na watendaji wa idara ya elimu kufanya ufuatiliaji wa nyumba kwa nyumba wote wasioripoti shule wanaripoti.

"Mkakati ulipo sasa ni kushirikiana na Mkurugenzi pamoja na wakuu wa shule na viongozi wengine kutoka kada ya elimu Sekondari kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shule ,hatakama mwanafunzi hana sare za shule atasoma huku mzazi wake akijipanga taratibu,tutafanya hivyo kutokana na sasahivi tunaanza mtaala mpya wa masomo kwahiyo wanaweza wasijekuelewa vizuri kwakuwa wenzao watakuwa wamefika mbali."Amesema Muumini.


Diwani viti maalumu kata ya Nyangamara Asha Nguli amesema kuwa changamoto kubwa ya wanafunzi kutoripoti shuleni nikutokana na hali ngumu ya maisha pamoja na umbali wa kutoka kwenye makazi yao yalipo pamoja na shule.

"Wanafunzi wengi wamekuwa wanachelewa kuripoti shule kutokana na umbali wa shule na makaazi yao yalipo,lakini sisi madiwani tunajitahidi sana kuhamasisha watoto kwenda shule,baadhi yao wamekuwa wakielewa lakini wengine hawaelewi kabisa, utakuta mzazi anasema mwanangu anasoma mbali akimaliza apati kazi."Amesema Nguli 

Post a Comment

0 Comments