HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA WAJA NA MKAKATI YA KUONGEZA MAPATO YA NDANI
Na Silvia Ernest,
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imekuja na mkakati wa ujenzi wa hosteli katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambayo itatoa huduma kwa wananchi ambao wamewaleta ndugu zao kuja kupata huduma za afya katika hospitali hiyo.
Mkakati huo umebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura katika ziara yake ya kutembelea Hospitali hiyo kukagua utoaji wa huduma za afya pamoja na ujenzi wa wodi tatu unaoendelea kutekelezwa.
Utekelezaji huu ambao utakuwa ni chanzo cha mapato ya ndani ya Halmashauri utaondoa adha kwa wananchi ambao wanalazimika kutafuta malazi maeneo mbalimbali ambayo yapo mbali na hospitali hiyo.
“Tumeona jinsi wagonjwa hasa hawa ambao wanaowasubiri ndugu zao ambao wamefika kujifungua wanalazimika kwenda mbali kutafuta malazi, ujenzi wa hosteli utasaidia kutoa huduma kwa gharama nafuu na kutatua changamoto hii" Amebainisha
0 Comments