JANUARI 28 MTWARA KUANZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


 JANUARI 28 MTWARA KUANZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Wananchi mkoani Mtwara wanatarajia kuanza kufanya maboresho katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo wametakiwa kutumia majukwaa mbalimbali katika kuwahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye zoezi hilo litakaloanza Januari 28 na kumalizika Februari 3 mwaka huu.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Tume na wadau wa Uchaguzi kuhusu zoezi la Uboreshaji wa daftari La kudumu La Wapiga Kura Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele.

"Ufanikishaji wa zoezi hili utategemea na mchango wa wadau katika kutoa elimu, ni matumaini yetu kuwa mtakuwa wadau wazuri wa kuhamasisha zoezi la Uboreshaji ili watu wajitokeze kuboresha taarifa zao” amesema Mhe. Mwambegele


Aidha Mhe Mwambegele amewasisitiza Mawakala wa Vyama vya siasa kutoingilia Mchakato wa zoezi zima la Uboreshaji wa daftari la kudumu badala yake amewasihi kufuata kanuni na miongozo iliyotolewa na kufanya mawasiliano na Tume pale inapotokea changamoto ili kuwekana sawa.

Ameendelea kutoa rai rai kwa wananchi kujiepusha na kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja huku akiwahimiza wadau waliohudhuria Mkutano huo kutoa ushirikiano Kwa Maafisa watakaoendesha zoezi hilo.


Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga unahusisha raia wa Tanzania wenye umri unaoanzia miaka 18 na zaidi na na watakaofikisha umri huo tarehe ya Uchaguzi ikifika, kutoa kadi mpya kwa Wapiga kura waliopoteza kadi au kuharibika , Kutoa fursa Kwa Wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao

Sifa zingine ni pamoja na Kutoa fursa Kwa Wapiga kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama waweze kuhamisha taarifa zao kutoka Kata au Jimbo walipoandikishwa awali pamoja na kuondoa Wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali.


Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka huu linaenda na Kauli Mbiu inayosema "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"

Post a Comment

0 Comments