KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA WANANCHI YAMPONGEZA RAIS SAMIA



 KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA WANANCHI YAMPONGEZA RAIS SAMIA.

*●Ni kwa kuleta maendeleo haraka nchini* 

#KAZIINAONGEA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa utendaji kazi wake kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Wananchi wa Tanzania yanavyopatikana kwa ufanisi mkubwa.

Hatua ya Kamati hiyo ya Bunge ya kumpongeza Rais wa Awamu ya Sita, imekuja kufuatia jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Samia, katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

Pongezi hizo zimetolewa Januari 21, 2025 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Fatma Toufiq wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya utekelezaji wa Mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Mashauri kwa njia ya Mtandao (Online Case Management System - OCMS) kwa Wananchi, kwa Kamati hiyo Jijini Dodoma.

Amesema, jitihada za Rais Samia katika kuwajali wananchi wake zinaendelea kuonekana na kwamba, Kamati hiyo ya Bunge imeona jitihada za uanzishwaji wa mfumo huo ambao utarahisisha katika usikilizwaji wa mashauri kwa haraka na wakati na Utasaidia kuwafikia watu wengi.

Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza pia Tume hiyo ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa uanzishwaji wa Mfumo huo wa  Uendeshaji na Usimamizi wa Mashauri kwa njia ya mtandao, ambao utarahisi utoaji huduma hiyo kwa Wananchi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla amesema, Mfumo huo upo mbioni kuzinduliwa na utaweza kuwaruhusu Wafanyakazi na waajiri kufungua mashauri wakiwa mahali popote bila kulazimika kwenda katika Ofisi za Tume kama ilivyokuwa hapo awali.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments