KAMISHNA WA UHIFADHI WA TFS ATEMBELE A SHAMBA LA MITI SAO HILL , ASISITIZA UWAJIBIKAJI NA USHIRIKIANO
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo @dos_silayo , ametembelea Shamba la Miti Sao Hill tarehe 11 Januari 2025, ambapo alizungumza na Menejimenti ya Shamba kuhusu utekelezaji wa shughuli za uhifadhi, ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti kwa msimu wa 2024/2025 katika Tarafa zote Nne za Shamba hilo.
Katika mazungumzo hayo yaliifanyika jana Januari 11, 2025, Prof. Silayo aliwakumbusha wahifadhi umuhimu wa uwajibikaji mahala pa kazi kwa kuhakikisha kuwa malengo yote yaliyopangwa kwa mwaka wa fedha yanatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Aidha, Kamishna alisisitiza kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya wahifadhi na wananchi ili kufanikisha juhudi za uhifadhi wa misitu kwa kiwango kikubwa zaidi.
“Ushirikiano ni nguzo muhimu ya mafanikio yetu, hivyo ni lazima tuendelee kushirikiana kwa karibu na jamii zinazotuzunguka,” alisema.
Shamba la Miti Sao Hill ni moja ya mashamba makubwa ya miti nchini yanayosimamiwa na TFS, likiwa na mchango mkubwa katika uzalishaji wa malighafi za misitu na kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu.
Mwisho
0 Comments