WANANCHI 1500 WA KIJIJI CHA MASHESE WAKATIWA BIMA YA AFYA
Mwandishi wetu-Mbeya
Serikali ya kijiji cha Mashese kata ya Ilungu wilayani Mbeya imetumia zaidi ya Sh 10 milioni kuwakatia bima za afya wananch1500 ili kuwa na uhakika wa huduma za kiafya na kujenga jamii imara.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mashese Osia Mwakalila amesema leo Januari 21,2025 huku akieleza kusudi la uongozi wake ni kuwafikia wananchi 2,000.
"Fedha hizo zilizotumika ni sehemu ya vyanzo vyetu vya mapato ya kijiji kulikaa na tukaamua kuwakatia bima za afya wananchi kutokana na baadhi yako kukosa huduma za matibabu kutokana na ukosefu wa kipato,amesema.
Mratibu wa Mfuko wa Bima ya Afya( CHF) Wilaya ya Mbeya Francisco Nguvila, amesema kilichofanywa na Serikali ya kijiji kuwakatia bima wananchi wake ni kitendo cha kuigwa na maeneo mengine kuhakikisha jamii inakuwa na afya imara na kuchochea maendeleo ya Taifa.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wameshukuru uongozi wa kijiji kwa kujali afya zao kwa kuwakatia bima za afya hali itakayo wawezesha kujikita katika shughuli za maendeleo wakiwa na afya njema.
Mwisho.
0 Comments