Korosho za Tanzania Kuelekea Sierra Leone: Ushirikiano Mpya wa Kilimo na Diplomasia*
Pembezoni mwa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), alikutana na Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mhe. Julius Maada Bio.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Naibu Waziri alimkabidhi Mhe. Rais wa Sierra Leone miche 130 ya korosho pamoja na kilo 20 za mbegu za korosho kwa ajili ya majaribio nchini Sierra Leone.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kushirikiana na nchi rafiki katika kukuza sekta ya kilimo ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Miche na mbegu hizo zinatarajiwa kusaidia Sierra Leone kuanzisha kilimo cha korosho kama zao la biashara hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya kilimo.
Tukio hili linaashiria uhusiano wa karibu kati ya Tanzania na Sierra Leone, hususan katika kushirikiana mbinu na teknolojia za kilimo bora.
0 Comments