MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WATOA HUDUMA KWA WANANCHI 500 DAR


MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WATOA HUDUMA KWA WANANCHI 500 DAR

#KAZIINAONGEA  

Madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wamepokea na kuwahudumia wananchi zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na maeno ya jirani Januari 13, 2025. 

Wananchi hao wamejitokeza kupata huduma za kibingwa za matibabu kutoka kwa Madaktari Bingwa na Mabingwa bobezi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hosptali ya Rufaa ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke .

Aidha, kambi ya matibabu ya kibingwa ambayo imeanza Januari 13,2025 imeshirikisha madaktari bingwa na mabingwa bobezi kutoka Hosptali za Rufaa za Mkoa za Amana, Mwananyamala, Ligula, Sokoine, Tumbi na baadhi kutoka Hosptali ya Taifa Muhimbili

Katikakambi hiyo, huduma za matibabu zinazotolewa kwa gharama nafuu ni katika magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Vipimo vya maabara na Mionzi, Magonjwa ya Ndani kama vile figo, Sukari, Moyo na shinikizo la damu).


Mengine ni magonjwa ya Kinywa na Meno, Ngozi, Macho, Magonjwa ya watoto, Afya ya Akili, Magonjwa ya Pua, Sikio na Koo.

Magonjwa ya mfumo wa Mkojo, Wataalamu wa Mazoezi Tiba na Viungo, Upimaji wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti pamoja na Magonjwa ya Mifupa.

Akizungumza kuhusu mwenendo wa zoezi hilo la kambi ya matibabu Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke Dkt. Joseph Kimaro amesema zaidi ya wagonjwa 500 wamepokelewa hadi kufikia saa 8 mchana huku wengine wakiendelea na huduma nyingine za matibabu


“Tunashukuru wagonjwa wanaendelea kuhudumiwa katika kambi hii ya madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia ambapo mpaka mchana huu wa siku ya leo tumewapokea zaidi ya wagonjwa mia tano na wote tunaendelea kuwahudumia kulingana na utaratibu tuliouweka, kambi imeanza lakini inatarajiwa kuzinduliwa rasmi hapo kesho Januari 14, 2025 na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila”, Amesema Dkt. Joseph Kimaro, Mganga Mfawidhi Hosptali ya Temeke.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments