Na Mwandishi wetu, Mbeya
Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini , Oran Njeza amesema serikali ya awamu ya sita imetekeleza vyema ilani ya uchaguzi tofauti na miaka mingine tangu nchi ipate uhuru.
Njeza amesema leo Jumatatu ,Januari 20,2024 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na namna serikali ya awamu ya sita ilivyo tekeleza ilani hususani katika sekta ya elimu,afya ,barabara sambamba na uchumi wa buluu kwa upande wa Zanzibar.
"Tunaona utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa vitendo ikiwepo miradi ya umeme,barabara,treni za kisasa za umeme ambazo kwa Tanzania tangu nchi ipate uhuru ni vitu vipya,"amesema Njeza.
Amesema kikubwa wanamshukuru Mungu kwani nchi ya Tanzania inakwenda vizuri kwa kufikia asilimia 99 ya maeneo ya vijijini wananchi vimefikiwa na nishati ya umeme huku maeneo ya vitongoji hatua mbalimbali zinaendelea.
Kuhusu elimu, Njeza amesema imeboreshwa ili watoto waweze kuwa na elimu bora yenye ushindani na kuwawezesha katika upatikanaji wa ajira ndani na nje ya nchi.
Amesema kufuatia kuvutiwa na utekelezaji wa ilani wajumbe wa Mkutano Mkuu waliokutana mjini Dodoma wameridhia kupitisha majina ya Rais Samia Suluhu Hassan kugombea tena katika uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Njeza amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameupiga mwingi kwa kugusa nyanya mbalimbali za kiuchumi na kuleta historia mpya ya Taifa la Tanzania.
Mwisho.
0 Comments