Mwandishi wetu, Mbeya
Walimu Wakuu 10 wa Shule za msingi jijini la Mbeya wapata motisha kwa kukamilisha kwa wakati miradi ya ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa na ukarabati kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri.
Motisha hizo zimekabidhiwa leo Ijumaa ,Januari 24,2025 na Ofisa Elimu Msingi Jiji ,Mwl Anderson Mwalongo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri John Nchimbi .
Ametaja sifa za walimu wakuu 10 waliopata motisha ni baada ya kukamilisha kwa wakati ukarabati wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa na ujenzi wa matundi ya vyoo kwa wakati
Mwalongo amewapongeza walimu wote kwa usimamizi mzuri wa miradi, huku akiwataka walimu wanaoendelea na ujenzi kukamilisha usimamizi huo ili kuendana na wakati.
Amesema ukamilishaji wa miradi kwa wakati unatufanya tutimize malengo ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan n Mbunge wa Jiji la Mbeya Dkt, Tulia Ackson pamoja na Balaza la Madiwani chini ya Mstahiki Meya wa Jiji Dormohamed Issa.
Kwa upande wake mratibu wa miradi ya shule Jiji, Abdallah Ally m amewataka walimu ambao hawajapata motisha waendelee kupambana kwenye usimamizi wa miradi ili wawe sehemu ya wapewa motisha.
Amesema katika kutekeleza miradi ya elimu kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024-2025 Halmashauri imetoa Sh 1.9 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa shule 25 za msingi vyumba 16 vipya vya madarasa, ukarabati wa vyumba 58 na ujenzi wa matundu 80 ya vyoo.
Mwisho
0 Comments