MKURUGENZI KASHUSHURA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MATIRI MBINGA

MKURUGENZI KASHUSHURA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MATIRI MBINGA

Na Silvia Ernest, Mbinga

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura amewataka watoa huduma wa Kituo cha Afya Matiri kutoa huduma bora za afya huku akisisitiza kuwa ongezeko la watoa huduma kituoni hapo liendane na utolewaji wa huduma bora za afya.

Hii ni baada ya Serikali kuajiri watoa huduma za afya nchini hivi karibuni na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa mnufaika wa ajira hizo.


Mkurugenzi huyo ametoa rai hiyo Januari 29, 2025 katika ziara yake ya kutembelea kituo cha afya Matiri kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

" Jumla ya watumishi nane wameongezeka hapa sasa kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha analeta tija kwa jamiii, hakikisheni mnafanya kazi kwa weledi" Amebainisha

Kwa upande wake Katibu wa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga George Mhina ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea jumla ya Watumishi 81 wa kada ya afya na Kituo cha Afya Matiri kimepokea watumishi 8.


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Matiri Mhe. William Mbwambo amebainisha kuwa ongezeko la watoa huduma limeleta tija kwa wananchi wa Matiri ambao awali walilazimika kwenda katika vituo vya afya binafsi au vilivyopo nje ya Kata hiyo jambo ambalo liliwaongezea gharama.

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo Jane Zackaria ameeleza kuwa awali kituo kilihudumia wagonjwa wapatao 400 kwa mwezi lakini sasa Kituo kinahudumia wagonjwa zaidi ya 600.

Post a Comment

0 Comments