MOI KUANZA KUSAJILI WAGONJWA KWAKUTUMIA NIDA


MOI KUANZA KUSAJILI WAGONJWA KWAKUTUMIA NIDA

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inapenda kuuarifu umma kwamba kuanzia tarahe 1 Februari 2025 itaanza usajili wa wagonjwa kwa kutumia namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Uamuzi huo unalenga kuboresha mfumo wa utambuzi wa wagonjwa, kuwa na taarifa zao kamili na kuweka kumbukumbu sahihi ili kuboresha utoaji huduma.

Pia kusaidia mifumo kusomana na kubadilishana taarifa za mgonjwa kwa. urahisi kutoka Taasisi moja ya kutolea huduma za matibabu kwenda sehemu zingine bila ya kuwa na mkanganyiko wa taarifa na kusaidia upatikanaji wa ndugu endapo mgonjwa atakua hatambuliki.

Hivyo Menejimenti ya MOI inawaomba wagonjwa wote wanaofika Taasisi ya MOI kupatiwa matibabu kufika katika dirisha la usajili wakiwa na Kitambulisho cha Taifa.

Aidha kwa wagonjwa ambao hawana kitambulisho cha Taifa, watatakiwa kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Sheha au kijiji anachoishi ambapo mwisho wa kupokea barua hizo itakua June 30, 2025.

Kwa wagonjwa wa dharura huduma itatolewa kwanza na utaratibu wa utambuzi utafanyika baadae na kwa watoto na wagonjwa kutoka mataifa mengine utaratibu uliopo utaendelea kutumika.

Post a Comment

0 Comments