MWANAFUNZI (19) MLEMAVU AJIUA KWA KUJIRUSHA KISIMANI MTWARA



    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara        SACP Issa Suleiman
 

Florence Sanawa, Mtwara
mtazamompyanews@gmail.com 

Mwanafunzi wa shule ya Wasichana Mtwara aliyefahamika kwa jina la Shadia Mussa (19) anaesoma Kidato cha Tano amejirusha kisimani na kupekeleka kifo chake huku chanzo cha kifo chake kikitajwa kuwa msongo wa mawazo.

Mwanafunzi huyo amejirusha katika kisima ambacho kipo katika shule hiyo. 

 Akizungumza na Waandishi wa habari  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. 

Amesema kuwa tukio hilo limetokea  Januari 25, 2025 ambapo amesema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na ulemavu wa viungo. 

Kamanda amesema kuwa kwa maelezo ya wanafunzi wenzake awali alionekana kuwa na mawazo kwa siku kadhaa kabla hakachukua maamuzi ya kujirusha kisimani. 

Aidha Kamanda huyo amesema Mkuu wa Shule hiyo alifanya jitihada kubwa za kujaribu kuzungumza na binti huyo mara kwa mara kutokana na hali ambayo walimuona nayo lakini jitihada hizo hazikuweza kusaidia hadi alipofanya maamuzi ya kujirusha kisimani. 

 #mtazamompyanews

Post a Comment

0 Comments