POLISI MBEYA YAWATUNUKU ASKARI 8 KWA UTENDAJI BORA 2024
Mwandishi wetu, Mbeya
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeadhimisha siku ya familia kwa kuwapa zawadi askari 8 waliofanya vizuri katika kukabiliana na makosa mbalimbali kama uharifu,ukatili na usalama barabarani mwaka 2024.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Benjamin Kuzaga amesema jana Januari 17,2025 katika viwanja vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU)ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu .
Kuzaga amesema hatua ya kuwatunuku vyeti na kuwapa zawadi askari 8 ni kutambua mchango wao katika kukabiliana na matukio mbalimbali yakiwepo ya uharifu na kufanya jamii kuishi kwa amani na usalama.
"Sio kwamba askari wengine hawafanyi kazi bali kamati ngazi ya Mkoa na Wilaya ilifanya utafiti wa kina na kuzingatia mwongozo wa Polisi Tanzania na kuwabaini 8 kati ya 1,000,"amesema.
Kuhusu hali ya usalama kwa mwaka 2023/24 Kuzaga amesema matukio ya uharifu yamepungua kwa kiwango kikubwa na kwamba utendaji mzuri wa kazi ndani ya Jeshi hilo umefanikisha.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amelipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo ya kutoa motisha kwani itaongeza chachu ya utendaji wa kazi.
Haniu amewataka askari polisi kuongeza weredi katika kuimarisha hali ya usalama wa nchi kwa raia na mali zao sambamba na kutaka vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuiga mfano huo.
Mwisho.
0 Comments