RAIS SAMIA AMLILIA MKUU WA WILAYA YA MBOZI
#KAZIINAONGEA
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameomboleza kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Mahawe aliyefariki dunia Januari 14, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) mkoani Kilimanjaro alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika salamu zake za maombolezo Rais Dkt. Samia ameandika: Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe, Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo Januari 14, 2025 katika hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.
“Nawapa pole familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi uhodari,ukweli na msimamo thabiti katika utendaji”.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments