RAIS SAMIA AMLILIA SHEIKH MUHAMMAD IDDI
#KAZIINAONGEA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za rambirambi kwa Mufti Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir kufuatia kifo cha Sheikh Muhammad Idd aliyekuwa Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mwinyiamani, Mshauri wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana na Mratibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, kilichotokea Januari 30, 2025.
Katika salamu zake hizo, Rais ameandika kwenye kurasa zake za kijamii kuwa: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Sheikh Muhammad Iddi (Abuu Iddi), Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mwinyiamani, Mshauri wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana na Mratibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, kilichotokea leo Alhamisi, Januari 30, 2025.
Natoa salamu za pole kwa familia, Mufti Mkuu wa Tanzania, Waislamu wote nchini, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Tumeondokewa na mtu aliyeipenda nchi yake, mwalimu katika imani, mlezi wa wengi katika imani, mpenda haki, mpenda ukweli, umoja, amani na utulivu wa nchi yetu, aliyetumia muda wake mwingi kuyasimamia na kufundisha hayo kupitia mawaidha yake.
Mwenyezi Mungu ampe Kauli Thabit, amsamehe makosa yake, amzidishie katika mizani mema aliyotenda, na ampe nafasi katika Pepo yake.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un."
#KAZIINAONGEA
0 Comments