RAIS SAMIA APONGEZWA KWA KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII NA BANDARI TANGA
#KAZIINAONGEA
Mkuu wa Mkoa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian amempongeza Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoifanya nchini ikiwemo mkoani humo na kufungua fursa za kiuchumi, ikiwemo upanuzi wa Bandari, hivyo kuongeza fursa katika Sekta ya Uwekezaji.
Balozi Dkt.Burian ametoa pongezi hizo Januari 19, 2025, mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) upande wa Zanzibar na Tanzania Bara, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, uliofanyika Mjini Dodoma Januari 18 na 19, 2025.
Balozi Dkt. Burian amesema Wanatanga wanashuhudia utendaji mkubwa katika huduma mbalimbali ikiwemo za kijamii na hata katika miundombinu, lakini pia suala zima la uchumi, na namna mkoa huo ulivyokuwa na mtazamo mzima wa upanuzi wa Bandari na mambo mengine makubwa yameweza kufanyika.
“Leo pale Tanga ukifika utakutana na Uwekezaji mkubwa wa bomba la mafuta ambalo litasafirisha Mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Jijini Tanga ambao utaufungua Mkoa wetu Kiuchumi na kuinua pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla na mradi huu ni muhimu kwa Maendeleo,” amesema.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments