RAIS SAMIA MWAMBA WA MAGEUZI YA KWELI BANDARINI


RAIS SAMIA MWAMBA WA MAGEUZI YA KWELI BANDARINI

#KAZIINAONGEA

Kama hukuwahi kufuatilia mwenendo wa utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam, huwezi kukubaliana na mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na kiongozi shupavu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakati mwanamama huyu anaingia madarakani hali ya utendaji kwa ujumla kwenye bandari hiyo ilikuwa ni ya wastani, mapato yalikuwa yanapatikana na huduma zinatolewa, lakini hazikuwa katika kiwango kilichopaswa kuwa.

Na hii ilikuwa inatokana na uchache wa vifaa na kasi nyonge ya watendaji wa bandari hiyo katika kupakiza na kupakua makasha.

Mara baada ya Rais Samia kuamua kuchukua  uamuzi mgumu ambao ulitawaliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa watu wa ndani na nje ya nchi ambao walikuwa wakinufaika na mwenendo ule wa awali, hali sasa ni tofauti.

Ajira rasmi na zisizo rasmi zimeongezeka bandarini, msongamano wa meli kuingia na kutoka  umeshuka kutoka wastani wa siku 48 hadi wastani wa siku tano.

Vifaa 10 vya kisasa vya kupakua kontena 31 kwa saa vimefungwa, hii inamaanisha kuwa kwa sasa upo uwezekano wa kupakua kontena 310 kwa saa.

Gharama ya kusafirisha makontena imeshuka kutoka wastani wa Dola 3,500 hadi Dola 2,000

Shehena zinazohudumiwa zimeongezeka kutoka tani 141,889 mwezi Mei 2024 hadi tani 168,336 mwezi Septemba 2024, sawa na ongezeko la asilimia 18.6 ndani ya miezi mitano.

Aidha mapato ya kodi yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni moja mwezi Septemba 2024, ikilinganishwa na wastani wa shilingi bilioni 850 kwa mwezi kabla ya uwekezaji wa DP World. 

Idadi ya makasha imeongezeka kutoka wastani wa 12,000 kwa mwezi hadi 27,000 mwezi Septemba 2024, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa katika historia ya bandari ya Dar es Salaam.

Hatua hiyo si tu imeleta tija kwa bandari ya Dar es Salaam pekee, bali imeleta tija kitaifa na kimataifa kwani kwa sasa wafanyabiashara wengi wanasafirisha na kupokea mizigo yao kwa haraka zaidi.

Hii iliisukuma hata nchi ya Rwanda kutoa pongeza kwa Mamlaka ya Bandari Nchini kutokana na uboreshaji huo mkubwa.

Hata hivyo mafanikio haya yanachagizwa zaidi ya kiu ya Rais Samia ya kutaka kuona tija inapatikana katika kila eneo la kibiashara nchini.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments