SERIKALI KUENDELEA NA MIKAKATI YA KUSIMAMAMIA USAFIRI WA ANGA NCHINI


SERIKALI KUENDELEA NA MIKAKATI YA KUSIMAMAMIA USAFIRI WA ANGA NCHINI

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejipanga kutekeleza mikakati yenye lengo la kuhakikisha kunakuwa na uendelevu wa kusimamia Sekta ya Usafiri wa Anga nchini kwa sasa na baadaye.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Salim Msangi wakati akiwasilisha mikakati hiyo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu 15, Januari, 2024 Mkoani Dodoma.

Mikakati hiyo ni pamoja na kuendelea kusimamia sheria na kanuni za usafiri wa Anga ili kuhakikisha Anga la Tanzania linaendelea kuwa Salama na kuwa kivutio kwa Mashirika ya Ndege ya Kimataifa na kuendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya Ukaguzi wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ambapo kwa sasa TCAA imeendelea kuhuisha kanuni za usafiri wa Anga ili ziendane na matakwa ya Shirika la Kimataifa la Usafiri huo Duniani, kuhuisha nyaraka na miongozo ya wakaguzi ili ziendane na mabadiliko ya kanuni mpya.

Ametaja mikakati mingine kuwa ni kuendelea kutoa mafunzo kwa ajili ya wakaguzi ili kupata weledi na namna bora ya kufanya kaguzi na usimamizi wa uthibiti wa Usafiri huo, na kuendelea kufanya kaguzi za ndani ili kutathimini uwezo wa kampuni zilizosajiliwa nchini kwa kuzingatia matakwa ya kanuni za Usafiri huo nchini na kuendelea kusimamia mafunzo endelevu kwa Marubani, Wahandisi, na Watendaji wengine wa Sekta ya Usafiri wa Anga.

Pia kuendeleza uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya uongozaji wa Ndege na mawasiliano, kuhakikisha inaendana na mabadiliko ya Kiteknolojia na matakwa na miongozo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), na kuendelea kushirikiana na nchi jirani na mashirika ya Kikanda na Kimataifa kwa kushiriki mikutano na makongamano kwa lengo la kubadilishana uzoefu.

“Mikakati mingine ni kuhimiza matumizi ya Teknolojia rafiki kwa mazingira katika Sekta ya Usafiri wa Anga kwa lengo la kupunguza athari za mazingira zinazotokana na shughuli za Anga, kuhakikisha viwanja vya ndege na miundombinu inayohusiana inakidhi viwango vya Kimataifa, lakini pia kuendelea kukitangaza Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) ili kuweza kuwavutia watanzania na wasio watanzania kujiunga na masomo ya muda mfupi katika sekta ya Usafiri wa Anga,” amesema.

Pia kuendelea na ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga ili kuweza kuwa na mazingira bora zaidi ya kufundishia pamoja na vifaa vya kisasa ambapo Kamati imesisitiza kusimamia mikakati hiyo na kuhakikisha chuo cha CATC kinajengwa.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments