SERIKALI KUFIKISHA HUDUMA YA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO KATIKA WILAYA 139


SERIKALI KUFIKISHA HUDUMA YA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO KATIKA WILAYA 139

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kufikisha huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 139 nchini.

Mpaka sasa Wilaya 108 tayari zimefikiwa huku  Wilaya 31 zilizosalia nazo zikitarajiwa kupata huduma ya mkongo wa Taifa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Pwani alipo tembelea na kukagua vituo vya Mkongo vilivyopo Chalinze, pamoja na kituo kipya  kilichojengwa Kibaha

Aidha, Mhandisi Mahundi  amempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa namna anavvyo anaendelea kuiwezesha sekta hii ya Mawasiliano hapa nchini kwa kuwekeza fedha nyingi katika Shirika la Mawasiliano  Nchini ( TTCL) na kuahakikisha  Shirika linajiendesha  kibiashara pamoja na kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali.

Aidha ameeleza kuwa Serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuelekea nchi jirani ya Congo (DRC) kupitia Ziwa Tanganyinga hadi Kalemei na tayari utekelezaji wake umeshaanza na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu mradi huu utakuwa umekamilika.

Sambamba na hayo, Mhandisi Mahundi  ameeleza kuwa kazi kubwa inaendelea kufanyika katika uwekezaji wa Mkongo wa Taifa ikiwa ni pamoja na kuunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini, kupitia SEACOM, EASSY na 2AFRICA.

"Na kwa kuzingatia tunajenga Tanzania ya kidijitali tunaunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini iliyopo Mombasa, Kenya kupitia Horohoro, Tanga, hii itasaidia kuongeza uhakika wa huduma ya Mawasiliano nchini.

"Endapo mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utakamilika utapanua wigo wa kibiahara ndani na nje ya nchi na kuongeza uchumi wa taifa."

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments