SERIKALI YA RAIS SAMIA YAPONGEZWA KUWAWEZESHA MAAFISA UGANI KIBAHA

 

SERIKALI YA RAIS SAMIA YAPONGEZWA KUWAWEZESHA MAAFISA UGANI KIBAHA

#KAZIINAONGEA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mji,  Dkt. Rogers Shemwelekwa, amesifu jitihada za Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Maafisa Ugani katika nyanja ya usafiri, na hivyo kuweza kuwafikia wakulima katika kutoa ushauri wa ugani Wilayani humo.

Akiongea wakati wa hafla za kukabidhi pikipiki 37 kwa Maafisa ugani Wilayani humo hivi karibuni, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa, kwa sasa kuna jumla ya Watumishi Ugani wa Kilimo 41,  wanaotoa ushauri wa ugani kwa wakulima 7, 528.

"Maafisa Ugani hawa wameweza kutoa ushauri kwa wakulima hao, katika mitaa yote 73 kutoka Kata 14, ambapo kwa sasa Halmashauri hiyo ina eneo linalofaa kwa kilimo lenye ukubwa wa wastani wa Hekta zipatazo 7,750 na kwamba, wakulima 3,600 tayari wameorodheshwa katika mfumo wa mbolea na mbegu za ruzuku katika msimu kwa mwaka 2024/2025 na wanapata mbolea na mbegu za ruzuku,  tunamshukuru Rais kuwawezesha usafiri katika kuendelea na majukumu yao,"amesema.

Ameongeza kuwa, hadi sasa  Halmashauri hiyo ina fursa mbalimbali na kuna wakulima 191 wa zao la korosho waliofanikiwa kupata ruzuku kwa ajili ya zao hilo, ambapo pia wakulima wapatao 6, 709 ni wale wa mbogamboga, na wakulima 628 ni wa mazao ya matunda.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments