SERIKALI YAFUNGUA FURSA KWA WANANCHI MKUTANO WA NISHATI AFRIKA


SERIKALI YAFUNGUA FURSA KWA WANANCHI MKUTANO WA NISHATI AFRIKA

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za kibiashara katika mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi za Afrika unaotarajiwa kufanyika Januari 27 na 28, 2025 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameweka wazi kuwa mikutano kama hiyo ni fursa kwa nchi na wananchi kujiongezea kipato kwani pamoja na ujio wa wakuu wa nchi,lakini pia kutakuwa na wataalamu mbalimbali na wasaidizi wao ambao watahitaji huduma mbalimbali.

Aidha Dkt. Biteko alielezea maendeleo ya maandalizi ya Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi 54 za Afrika, Mawaziri wa Fedha na Nishati, pamoja na Marais wa Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

 “Uteuzi wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa ni matokeo ya juhudi za diplomasia za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,” ameongeza Dkt. Biteko.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments