SERIKALI YAITAKA CAMARTEC KULETA MABADILIKO SEKTA YA KILIMO


SERIKALI YAITAKA CAMARTEC KULETA MABADILIKO SEKTA YA KILIMO

*●Ni katika uzalishaji na uthibiti wa zana za kilimo*

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imeiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa  Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC), kuleta mabadiliko zaidi katika uzalishaji na udhibiti wa zana za kilimo zinazoingia kutoka nje ya nchi ikiwemo kutopata hati chafu sanjari na matumizi sahihi ya fedha. 

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ameyasema hayo Januari 24, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa CAMARTEC, Jijini Arusha ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo amekula kiapo cha Maadili.

Dkt. Jafo ameisisitizia Bodi hiyo kusimamia vema kazi za kituo hicho ikiwemo kuacha  kufanya kazi kwa mazoea  ili kuhakikisha zana za kilimo zinawafikia wananchi wengi hususani wakulima ili waweze kuwa na matumizi sahihi ya zana za kilimo na vema ili kuhakikisha CAMARTEC inapata maendeleo ambapo pia ameishauri Bodi hiyo kuendelea kutoa ushauri ikiwemo kusimamia Menejinenti na Wajumbe  wake, kufanya kazi kwa upendo na nidhamu kazini ili kuhakikisha wanaleta tija katika kituo hicho na kuhakikisha wanatoa matunda bora.

Aidha, amezitaka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake  ikiwemo CAMARTEC, kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili  ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kiweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika kuelimisha umma kuhusu jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta ya viwanda na biashara. 

Naye Mkurugenzi wa  Sera na Mipango kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya akimwakilisha  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt,Hashil Abdalah amesema, anaamini Bodi hiyo itasimamia kwa ukamilifu tafiti na majaribio ya Teknolojia kwa ajili ya zana za kilimo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchini

Akisoma taarifa ya kituo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama amesema  Kituo hicho kimefanikiwa kuunda zana mpya 42 zinazozalisha zana mbalimbali kwa ajili ya  kuongeza tija katika kilimo.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya CAMARTEC, Prof.  Valerian Silayo amesema kuwa, Bodi hiyo imepokea maelekezo yote yaliyitolewa na iko tayari kuyafanyia kazi ili  kuhakikisha CAMARTEC inafikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kusaidiwa upatikanaji wa fedha za kuendesha kituo hicho kwa wakati.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments