#KAZIINAONGEA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Afya, imeutaka Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuhakikisha mapato ya mfuko huo, yanatumika vizuri kwa kazi zinazotambulika, kufanya kazi kwa karibu na Sekta Binafsi ili kusaidia kuongeza juhudi kwenye Sekta ya Afya pamoja na kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu vifurushi walivyokubaliana na vinavyofanya kazi kwenye Bima ya Afya kwa wote.
Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Januari 21, 2025 Jijini Dodoma.
Waziri Mhagama amesema kuwa, Viongozi hao wahakikishe mafanikio haya ambayo yamefanya mfuko kuwa na ziada ya mapato, yanayotumika vizuri kwa kazi zinazotambulika na kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na matumizi halisi ya mapato ambayo Mfuko umejipatia.
"Eneo lingine niendelee kuwakumbusha kufanya kazi kwa karibu na Sekta binafsi, kwa sababu tunaichukulia kama Sekta itakayosaidia kuongeza juhudi kwenye Sekta ya Afya, na sio kuwachukulia kama washindani kati ya Sekta za Umma na Sekta binafsi, kwani zipo Hospital kubwa za Sekta binafsi zinazofanya vizuri na kuleta mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Afya, hivyo ni vyema kushirikiana nao," amesema Mhagama.
"Pia eneo lingine ni kuhakikisha vifurushi vile ambavyo tulikubaliana na vinafanya kazi vinaendelea kutolewa elimu na kusimamiwa vizuri ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi," amesema.
Bodi hiyo ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), imezinduliwa na Waziri wa Afya Jenista Mhagama ni Bodi ya 6 tangu kuanza kwa Bodi za Mfuko huu.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments