SERIKALI YAITAKA RUWASA KUKAMILISHA MRADI WA KISIMA IFIKAPO JANUARI 31


SERIKALI YAITAKA RUWASA KUKAMILISHA MRADI WA KISIMA IFIKAPO JANUARI 31

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imemtaka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Ruangwa (RUWASA), kukamilisha uchimbaji wa kisima cha maji katika Kijiji cha Mmawa, ifikapo 31, Januari, 2025 ili  maeneo yote ambayo hayajakamilika kutoa huduma ya maji, yaanze kutoa huduma hiyo kama dhamira ya Serikali ilivyotarajia.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji Kijiji cha Mmawa, Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Methew amesema,  Mamlaka hiyo ya Maji inapaswa kukamilisha Mradi huo wa maji kwa wakati, ili kuwaondolea adha Wananchi wa maeneo hayo na maeneo jirani.

Aidha, Kundo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa uchimbaji visima na ujenzi miundombinu rahisi wa Shilingi Milioni 325 katika vijiji vitano Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

Pia ameeleza kuwa Serikali ya Rais Samia, inaendelea kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi ya maji lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi, ambapo pia amemtaka Mhandisi wa Maji kuhakikisha anafanya maboresho katika baadhi ya maeneo ikiwa pamoja na mita na presha ya utokaji wa maji kwenye mabomba.

Mradi huo wa uchimbaji visima na ujenzi wa miundombinu rahisi katika vijiji vitano ambavyo havina huduma ya maji, ni programu maalumu ya Serikali ya uchimbaji visima 900 inatekelezwa nchi mzima katika Majimbo yote ya Uchaguzi.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Ruangwa Lawrence Mapunda amesema, mradi huo unatekelezwa kwa kutumia force akaunti ambapo ujenzi wa miundombinu kwa sasa umefikia asilimia 85.

Mradi huo utakapokamilika utawanufaisha jumla ya kaya 917 kutoka katika vijiji vitano ambavyo ni Mmawa, Mtawilile, Njawale, Mpara na Namkatila huku ikiongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kwa asilimia 2.62 kutoka asilimia 74.8 hadi kufikia asilimia 77.42 ambapo miradi hiyo itakapokamilika itaendeshwa na kusimamiwa na Wananchi wenyewe kupitia vyombo vya watumia maji.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments