SERIKALI YAITAKA TARURA KUCHIMBA KISARAWE ZAHANATI YA BWAMA KISARAWE


SERIKALI YAITAKA TARURA KUCHIMBA KISARAWE ZAHANATI YA BWAMA KISARAWE


#KAZIINAONGEA

Serikali ya awamu ya Sita kupitia Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mkoa wa Pwani, Dkt.Selemani Jafo, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe kuziagiza Taasisi za RUWASA kuhakikisha wanachimba kisima katika Zahanati ya Bwama Wilayani humo.

Dkt. Jafo amesema, kisima hicho kitasaidia upatikanaji wa maji katika Zahanati na matumizi kwa Wananchi pamoja kuiagiza TARURA kuhakikisha barabara inayounganisha kijiji hicho inafanyiwa ukarabati kwa haraka pamoja na kuagiza Taasisi zote zishiriki katika ziara zake.

Aidha, Dkt.Jafo amesema Serikali kuwa, kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kuwajali wananchi wa Kisarawe kwa kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa kujenga miundombinu ya huduma hizo kwenye kila Kata na Vijiji kama vile afya, nishati na elimu katika jimbo hilo la Kisarawe kwani karibia Kata zote zimefikiwa.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments