SERIKALI YAJENGA KILOMETA 13,991 ZA MKONGO WA MAWASILIANO ZINAZOUNGANISHA MIKOA YOTE NCHINI


SERIKALI YAJENGA KILOMETA 13,991 ZA MKONGO WA MAWASILIANO ZINAZOUNGANISHA  MIKOA YOTE NCHINI

*●Kuanza kutumika Februari, 2025*

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Awamu ya Sita  chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imefanikiwa kujenga jumla ya Kilometa 13,991 za Mkongo zikiunganisha Mikoa yote ya Tanzania Bara, Wilaya 109, pamoja na nchi saba (7) zinazopakana na Tanzania.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), CPA Moremi Marwa, 23, Januari, 2025 wakati akimkaribisha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, kukagua Mradi wa ufikishaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Mombasa, kupitia Kituo cha Horohoro kilichopo Wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga.

Maunganisho hayo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano yatawezesha Mkongo wa Taifa kuunganishwa na Mikongo ya Baharini iliyopo katika Pwani ya Mombasa na kwamba, hadi kufikia Desemba 2024 tayari walikuwa wamekamilisha ujenzi wa Mikongo hiyo kwa nchi hizo zilizopakana na Tanzania ambazo ni nchi ya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, na Msumbiji.


Akikagua Mradi huo, Waziri Silaa amesema kuwa, uwepo wa Kituo hicho cha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kinachounganisha Tanzania na nchi ya Kenya, kutachochea shughuli za kiuchumi kati ya nchi hizo mbili pamoja na nchi nyingine za jirani.

“Leo tumekuja hapa kuona kazi kubwa iliyofanyika ya kutengeneza njia mbadala ya Mkongo ambao unaunganisha nchi yetu na nchi ya Kenya kupitia hapa Horohoro kwenda Mombasa, Kenya na kuongeza kuwa kazi ya njia hii inaenda kufanya Mkongo wetu wa Taifa wa Mawasiliano kuwa na njia ya Dar es Salaam ambayo inaunganika na Mikongo ya Mawasiliano ya chini ya Bahari, lakini sasa kutakuwa na njia mbadala ya kuunganisha Mkongo wa Taifa na mtandao wake na mikongo saba ya chini ya Bahari iliyopo Mombasa,” amesema Waziri Silaa.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments